Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Biashara na Uchumi / Ukosefu wa viwanda wachochea magendo katika Ngozi.

Ukosefu wa viwanda wachochea magendo katika Ngozi.

Na Mariam Emily,

Bukoba.

 

Tanzania ni nchi ya pili nyuma ya ETHIOPIA kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo barani Afrika ikiwa na ng’ombe zaidi ya milioni mia nne mbuzi zaidi ya milioni kumi na tano na kondoo milioni saba lakini ikiwa imezidiwa katika sekta ya usindikaji wa ngozi na nchi jirani,hali inayoonyesha wazi kuwepo na mianya ya magendo ya malighafi hiyo katika mipaka yake.

 

Hayo yalibainika katika warsha ya wadau wa mifugo iliyofanyika mjini Bukoba, lengo likiwa ni kuhusu uanzishwaji wa mfumo wa ufuatiliaji wa uzalishaji wa malighafi ya ngozi kutoka machinjioni hadi viwandani.

 

Baadhi ya maafisa wa mifugo kutoka wilaya mbalimbali mkoani humo,walielezea changamoto kubwa wanayoipata ikiwemo kuingiliwa na wanasiasa katika utendaji wao wa kazi,hatua inayotajwa kama kikwazo katika kuzuia magendo ya zao la ngozi katika maeneo ya mipakani hoja inayojibiwa na Afisa Ufatiliaji kutoka TAMISEMI ,Leo Mavika

 

Nao uongozi wa Mkoa wa Kagera umeahidi kushirikiana na wadau wote kudhibiti biashara ya magendo ya ngozi hatua  inayolipunguzia taifa mapato.

 

Kisha  wataalam hao  kutoka wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi walitembelea machinjio ya Manispaa ya Bukoba eneo la Rwamishenye,na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara wa ngozi ambapo wafanyabiashara hao  wamekiri kuwepo na biashara ya magendo ya ngozi nje ya nchi kutokana na upungufu wa viwanda vilivyopo hapa nchini na hivyo kuwalazimu baadhi yao kutafuta wanunuzi nje ya nchi.

 

 

Licha  Tanzania kuwa nchi ya pili kwa kuwa na mifugo mi  ngi barani Afrika, Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya usindikaji wa mazao yatokanayo na mifugo kutokana na kutokuwepo kwa viwanda vya kutosha hali inayosababisha kuwepo na magendo ya malighafi hizo kwenda nchi jirani.

 

Kuhusu admin

Check Also

KAZI ZA SANAA NCHINI: Utafiti duni wachangia kushusha ubora wake

Katibu mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso anasema wasanii wa maigizo nchini hawana …

WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

Mkuu wa mkoa wa Mara Dokta Charles Mulingwa amewataka wawekezaji waliouziwa viwanda na serikali mkoani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *