Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Uongozi  wa machinjio ya Vingunguti walalamikiwa

Uongozi  wa machinjio ya Vingunguti walalamikiwa

Wafanyabiashara wa Machinjio ya Vingunguti jijini Dar es salaam wameulalamikia Uongozi wa Chama cha Umoja wa Wafanyabiashara wa Mifugo na Mazao yake Vingunguti (Uwamivi) kuwa chanzo cha mgogoro kwa sababu ya kukiuka makubaliano ya pamoja.

Wafanyabiashara hao wamedai kufanya shughuli zao katika mazingira magumu licha ya kuwepo kwa utaratibu mzuri wa uchinjaji ng’ombe  sambamba na uuzaji wa damu inayokadiriwa kuingiza shilingi milioni 18 kwa mwezi ambazo hazijulikani zinapokwenda.

Wafanyabiashara hao wamedai kutokuwa na wana imani na uongozi wa Chama hicho kwa madai ya kwenda kinyume na makubaliano ya taratibu za uchinjaji sambamba na kutofanyika kwa mikutano ya kujua mapato na matumizi na hivyo kuiomba Serikali iwasaidie kutatua tatizo lao.

 Hata hivyo, Startv ilimtafuta mtuhumiwa mkuu ambaye ni Mwenyekiti wa Uwamivi, Anatory Lubeli ambaye amekanusha madai hayo na kutolea ufafanuzi wa baadhi ya kanuni anazodai anazisimamia kikamilifu ziliwekwa na manispaa.

 Chama hicho cha Uwamivi kilianzishwa kwa lengo la kuwaletea Maendeleo na nguvu ya pamoja ya kujinufaisha wafanyabiashara hao, lakini kwa sasa wamedai kuwa chanzo cha migogoro tofauti na lengo la chama kilichoanzishwa mwaka 2012 na kusajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani.

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Maoni

  1. I see you don’t monetize your site, don’t waste your
    traffic, you can earn extra bucks every month because you’ve got hi quality content.
    If you want to know how to make extra money, search for: Mrdalekjd methods for
    $$$

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *