Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Michezo na Burudani / USAJILI DIRISHA DOGO:Stand United kusuka kikosi na kutangaza kocha mpya.

USAJILI DIRISHA DOGO:Stand United kusuka kikosi na kutangaza kocha mpya.

Ikiwa siku chache baada ya Shirikisho la Soka Nchini TFF kutangaza kufunguliwa kwa  dirisha dogo la usajili  kwa timu  za ligi kuu, Timu ya Stand United imesema itafanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake pamoja na kutafuta kocha kufuatia aliyekuwa kocha wa timu hiyo Patrick Lewig kuachia ngazi.Mwenyekiti wa timu hiyo Dokta Elison Maeja ameiyambia Star TV kwamba pamoja na ukata wa fedha za mfadhili lakini watatumia fedha za wadhamini kukisuka kikosi chake ili kiwe tishio kwenye mzunguko wa pili, Na katika mechi ya ligi ya vijana chini ya miaka 20 iliyopigwa kwenye uwanja wa Kaitaba, timu za Mwadui FC na Stand United zimetoka  sare  ya bao 1-1, bao la Mwadui likufungwa na Hassan Karata dakika ya 42 na Stand United likifungwa na Adam Salamba dakika ya 62.

Dk Maeja anasema bench la ufundi la timu yake linatarajia kufanya marekebisho makubwa kwa kuongeza wachezaji ili kukisuka kikosi cha CHAMA LA WANA, anasema watatumia  fedha wanazopata kwa wadhamini wa ligi kuu ya Vodacom ili kufanya usajili wa wachezaji wapya na zingine zitachangwa na wadau. Je? kuhusu ufadhili wa timu hiyo Dk Maeja anatoa wito kwa makampuni kujitokeza  kuifadhili  timu yake ili iweze kushiriki vyema mzunguko wa pili wa ligi kuu.Timu ya Stand imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa imeshika nafasi ya Sita na point 22 huku tayari ikiwa imevichapa vigogo Timu za Yanga na Azam.

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Kuimarishwa uwanja wa Nyamagana

Mipango ya kuendeleza soka la vijana huenda ikawa na tija endapo tu serikali chini ya …

• SHERIA 17 ZA SOKA: Waamuzi walaumiwa kuziweka

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara, ikifikia tamati ya mzunguko wa kwanza, mashabiki wa soka wametoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *