Tuesday , October 17 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / UTOAJI HUDUMA ZA MAJI: Bodi zitakazoshindwa kusimamia hatarini kufutwa

UTOAJI HUDUMA ZA MAJI: Bodi zitakazoshindwa kusimamia hatarini kufutwa

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema atazifuta bodi za mamlaka za maji bila kusubiri kipindi chake kumalizika endapo sheria za bodi hizo hazitasimamia utoaji wa huduma bora ya maji  kwa wanachi na ujenzi wa miradi ya maji yenye tija kwa wananchi na taifa.Mhandisi Lwenge amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa bodi ya mamlaka ya maji safi mkoani Mwanza MWAUWASA itakayodumu kwa kipindi cha miaka 3.

Ni asilima 50 wakazi ambao hupata maji safi na salama huku asilimia 23 wakiunganishwa katika mtando wa maji taka mkoani Mwanza na asilimia iliyobaki maji taka hutiririsha Ziwa Victoria hasa wakazi wa maeneo ya milimani.Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema serikali kwa kushirikiana na mamlaka ya maji MWAUWASA imeandaa mpango wa kuweka mtandao wa maji taka kwa wakazi wanaoishi milimani ikiwa makakati wa  kudhibiti uchafuzi mazingira katika Ziwa Victoria.

Waziri Mhandisi Lwenge amebainisha kuwa Mamlaka ya maji mkoani Mwanza kwa kushirikiana na wizara yake ina miradi kumi ya maji inayotazamiwa  kuondoa tatizo la maji katika wilaya ya Nyamagana na Ilemela.

Aidha Mhadisi Lwenge anaelezea mpango wa Serikali katika maeneo ya kanda ya ziwa.

Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mwanza MWAUWASA katika taarifa yake ya mamlaka kwa kipindi cha miaka 3 amesema mpaka sasa mamlaka hiyo inawateja 65000 na wanamtarajio ya kufikia wateja 70000 kukuamilka kwa miradi wanayojenga.

Mwenyekiti wa bodi ya maji MWAUWASA Christopher Mwita Gachuma na badhi ya viongozi wa Wamesema mamlaka hiyo imejipanga kuhakikisha Mwanza inafikia malengo ya kuondoa tatizo la maji katika maeneo ya nje ya miji na milimani.

Uzinduzi wa bodi hiyo uliambatana na ukaguzi wa miradi kumi ya maji inayojengwa na mamlaka ya maji safi na mazingira MWAUWASA na kuzindua mradi wa maji Bugando unaotazamiwa kuhudumia wakazi elfu  24 waliko katika milima ya Bugando kata ya Mahina unaojengwa kwa fedha zinazotolewa mamlaka hiyo.

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *