Wachimbaji wadogo wadhahabu washuriwa kujiunga na ujasiriamali

Wachimbaji wadogo wadhahabu washuriwa kujiunga na ujasiriamali

- in Biashara na Uchumi
Picha ya maktaba

WACHIMBAJI wadogo wadogo wa dhahabu wa mgodi ulioko katika kijiji cha Nyasana kata ya Kabasa Wilaya ya Bunda, mkoani Mara wameshauriwa kujiunga kwenye  ujasiriamali ili halmashauri ya Mji wa Bunda na serikali kwa ujumla iweze kuona namna ya kuwawezesha ili wajiinue kiuchumi.

Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Bunda, Abrahamu Mayaya, wakati akifungua ofisi ya kijiji hicho, ikliyojengwa kwa mchango mkubwa uliotolewa na wachimbaji wadogo wadogo, kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho kwa thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9.5.

Picha ya maktaba

Mheshimiwa Mayaya ambaye pia ni diwani wa kata hiyo, amesema kuwa serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na wachimbaji wadogo wadogo, katika suala zima la kuchangia miradi ya maendeleo na akawaomba wachimbaji hao wajiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ili waweze kujiinua kiuchumi.

Amesema kuwa kutokana na wachimaji hao kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo, halmashauri ya Mji wa Bunda pamoja na serikali kwa ujumla, itafanya kila liwezekanalo kwa kuunga mkono juhudi za wananchi hao, ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati kijijini hapo ili wananchi waweze kupata huduma za amatibabu kwa ukaribu zaidi.
Hata hivyo anasisitiza viongozi kujenga tabia ya kuwasomea wananchi mapato na matumizi juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Dismas Mathindo, anasema kuwa katika ujenzi wa ofisi hiyo wachimbaji wadogo wadogo katika mgodi huo, wamechangi kwa kiasi kikubwa.

Makamu mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wadogo katika Wilaya ya Bunda, Georges Miyawa na mwenyekiti wa wachimbaji hao katika mgodi huo Justine Raphael, wanaiomba serikali kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wachimbaji hao, kwani ni wadau wakubwa katika suala zima la kuchangia miradi ya maendeleo.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Majaliwa: Viwanda havitasimama kwasababu ya migogoro

SERIKALI imesema kuwa haita kubali kuendelea kusimamisha viwanda