Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Wakazi Mekomariro Bunda waiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi.

Wakazi Mekomariro Bunda waiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi.

Wakazi wa kijiji cha Mekomariro kata ya Mihingo wilayani Bunda mkoani Mara wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu kati yao na kijiji cha Sirorisimba wilayani Butiama ili kuepusha mapigano yanayoweza kutokea katika eneo hilo.

Mgogoro huo unadaiwa kuwa ni wa muda mrefu na umekuwa ukipigwa danadana na uongozi wa juu bila sababu za msingi kukiwepo baadhi ya viongozi kutokujali matatizo ya wakazi wa maeneo hayo.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mikomarilo kata ya mihingo wilayani Bunda Mkoani Mara, wamelalamikia uwepo wa mgogoro kati yao na wenzao wa kijiji cha Sirolisimba kilichopo wilayani Butiama baada ya kutwaa Ardhi yao na kumpa mwekezaji na kuanza kuitumia bila ridhaa yao.

Aidha wamesema kuwa tatizo la mgogoro huo wa ardhi unakuzwa na viongozi wa vijiji hivyo huku viongozi wakuu wakishindwa kuushughulikia.

Kwa upande wao mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho na diwani wa kata hiyo,Nyambura Nyamuhanga,wamesema kuwa mipaka ya kijiji hicho toka mwaka 1971 imekuwa ipo sawa lakini ubadilishaji wa mipaka ndo chanzo cha tatizo.

Mgogoro wa kijiji cha Mikomarilo kilichopo wilayani Bunda na Kijiji cha Siroli simba kilichopo wilayani Butiama mkoani Mara, umedumu kwa miaka zaidi ya Therathini kutokana na kila mara viongozi kuushughulikia na kutokuwepo kwa makubaliano ya wakazi wa vijiji hivyo viwili.

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *