Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Biashara na Uchumi / Wakazi wa Bwisya Ukerewe waanza kunufaika na umeme wa jua.

Wakazi wa Bwisya Ukerewe waanza kunufaika na umeme wa jua.

Wakazi wa kijiji cha Bwisya katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wamenufaika na mradi wa umeme wa jua unaotajwa kuwa kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi kupitia shughuli za uzalishaji mali na matumizi ya familia.

Mradi huo unatekelezwa na shirika la umeme Rural Power Supply Ltd ambalo linaundwa kwa ubia baina ya Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino na kampuni ya Inensus kutoka nchini Ujerumani.

Kisiwa cha Ukara ni miongoni mwa maeneo mengi ya Tanzania yaliyo nje ya grid ya taifa ya umeme. Hivyo Kwa miaka mingi nishati ya umeme imekuwa adimu kwa wakazi hao.

Makamu Mkuu wa Chuo SAUT Padre Thadeus Rwamkama na Mkuu wa Maliasili Umoja wa Ulaya Gianluca azzoni wamesema Mradi huo umegharimu bilioni 38.4 za kitanzania asilimia hamsini ya fedha hizo ni msaada kutoka umoja wa Ulaya, malengo ya kampuni ya Jumeme ni kuwafikia watu milioni moja ndani ya Tanznaia kupitia mitambo 300 katika vijiji vilivyo nje ya grid ya taifa ifikapo 2022.

 Matokeo ya mradi huo yanatajwa kama jitihada za Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kuleta mapinduzi ya nishati na matumizi ya umeme katika maeneo ya vijijini husasani yaliyo nje ya grid ya taifa.

 Ujumbe wa wawekezaji na wafadhili ni muitikio chanya wenye kujenge mahusiano yenye tija kwa jamii ya watanzania katika hatua za maendeleo.

Mapinduzi ya nishati kisiwani hapo huenda yakafungua milango ya uwekezaji katika sekta ya viwanda vidogo na vikubwa katika kuchakata mazao ya kilimo na samaki huku fursa za kibiashara na ajira zikitengenezwa miongoni mwa wakazi wa kisiwa hiki katika hatua za kuelekea uchumi wa kati.

 

 

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

KAZI ZA SANAA NCHINI: Utafiti duni wachangia kushusha ubora wake

Katibu mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso anasema wasanii wa maigizo nchini hawana …

WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

Mkuu wa mkoa wa Mara Dokta Charles Mulingwa amewataka wawekezaji waliouziwa viwanda na serikali mkoani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *