Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Biashara na Uchumi / Wakulima Njombe wadai kupunjwa na walanguzi

Wakulima Njombe wadai kupunjwa na walanguzi

Wakulima nchini wataendelea kupunjwa na walanguzi wanaonunua mazao kwa ujazo wa Lumbesa endapo Serikali haitaweka mikakati thabiti ya kuzuia ujazo huo kwa nchi nzima.

Kukosekana kwa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo vya mizani wakati wa uuzaji wa mazao ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuwapa nguvu walanguzi kuendelea kuwapunja wakulima.

Ujazo wa Lumbesa ni miongoni mwa changamoto inatajwa kuendelea kuwanyonya wakulima, na kuwakwamisha kuendesha kilimo cha kisasa ambacho kinachohitaji fedha ili kumudu gharama za ununuzi wa pembejeo za kisasa na mbegu bora za kilimo.

Wanunuzi wa mazao ya wakulima wananyooshewa kidole kuwa wao ndiyo sababu ya anguko la uchumi kwa wakulima na hiyo ni kutokana na wao kunufaika na ujazo huo mkubwa wa Lumbesa.

 Wakulima wa zao la Viazi mkoani Njombe nao ujazo huo wa Lumbesa wamesema ni kikwazo kwao, kwakuwa nao wanalazimika kuuza Viazi vyao kwa bei ndogo kwa kutumia ujazo badala ya vipimo.

Uongozi wa sekta ya kilimo Wilaya ya Njombe umekiri kuwepo kwa changamoto ya ujazo wa Lumbesa, na kuwa hilo ni tatizo la soko huria.

 Hata hivyo kukosekana kwa soko la uhakika juu ya mazao ndiyo sababu ya wakulima kuuza mazao yao kwa rihaa ya mnunuzi- ambapo mradi wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za Viazi Mviringo mkoani Njombe- SAGCOT umejipanga kuwakwamua wakulima wa zao la Viazi mviringo kwa kuwaepusha na changamoto ya soko.

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

KAZI ZA SANAA NCHINI: Utafiti duni wachangia kushusha ubora wake

Katibu mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso anasema wasanii wa maigizo nchini hawana …

WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

Mkuu wa mkoa wa Mara Dokta Charles Mulingwa amewataka wawekezaji waliouziwa viwanda na serikali mkoani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *