WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

- in Biashara na Uchumi

Mkuu wa mkoa wa Mara Dokta Charles Mulingwa amewataka wawekezaji waliouziwa viwanda na serikali mkoani humo kurejea na kuvifungua haraka kabla ya kuchukuliwa hatua kwa kitendo cha kupingana na agizo la Rais la wale wote waliouziwa viwanda kuvifungua kutokana na kuvigeuza maghala ya kuhifadhia mali zao.

Ametoa agizo hilo wakati akikagua uwekezaji mpya wa kiwanda cha maji cha Serengeti mjini Musoma kutokana na kuwepo kwa taarifa juu ya mwekezaji wa kiwanda cha nguo cha New Mutex kufungua mashine za kutengeza nguo na kuzihamisha.

Kiwanda cha nguo cha New Mutex ni kiwanda pekee kinachozalisha nguo kutokana na uwepo wa kilimo cha zao la pamba katika mkoa wa Mara.

Kiwanda hicho kimekuwa kikikumbwa na matatizo ya mara kwa mara na kusababisha mwekezaji kudaiwa kuanza kuondoa mashine zilizopo na kuzihamisha huku serikali mkoani humo ikiwataka wawekezaji kufika na kuwekeza.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha maji ya kunywa cha Serengeti mkuu wa mkoa wa Mara, Dokta Charles Mulingwa amesema kuwa mkoa huo ni salama kwa uwekezaji.

Nae mkuu wa wilaya ya Musoma na msimamizi wa kiwanda cha maji ya kunywa cha Serengeti, Magubo Joseph wamesema kuwa kukamilka kwa kiwanda hicho kutakuza pato la mkoa huo.

Mkoa wa Mara,umeanza kampeni ya kuufanya mkoa huo kuwa na viwanda ili kuitikia agizo la serikali ya awamu ya tano kuwa nchi ya viwanda.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Majaliwa: Viwanda havitasimama kwasababu ya migogoro

SERIKALI imesema kuwa haita kubali kuendelea kusimamisha viwanda