Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Wananchi wa Mtwara vijiji wamlilia Simbachawene.

Wananchi wa Mtwara vijiji wamlilia Simbachawene.

Na Joseph Mpangala,

Mtwara.

 

Wakazi wanaoishi kandokando ya visima vya kuchimba na kuchakata nishati ya Gesi eneo la ziwani mkoani Mtwara wameilalamikia Serikali kwa kukosekana kwa umeme katika vijiji vyao ingawa nishati hiyo inachimbwa miongoni mwa vijiji hivyo.

Wakazi hao wamelalamikia hali hiyo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene wakati akifanya ziara yake katika kiwanda cha kuchakata Gesi kilichopo Mnazi bay kutokana na kunusurika na kusombwa na maji ya Bahari.

Katika ziara ya siku moja kwenye kiwanda cha kuchakata gas cha M n P  kilichonusurika kuchukuliwa na maji mwanzoni mwa January mwaka huu na kulazimika kutumi Jeshi la wananchii kuongeza michanga pamoja na mawe katika ukingo wa bahari ili kuzuia maji yasiendelee kuchukua ardhi iliyobaki mita 28 kufika katika kiwanda hicho kinachozalisha Gas kwa ajili ya umeme wa mikoa ya Lindi na Mtwara.

Wenyeviti wa vijiji vya Luvula na mnuyo wakatoa malalamiko yao kwa waziri nishati na madini George Simbachawene kuwa wanahitaji kutazamwa kutokana na baadhi ya wakazi  mazao yao yalikatwa ikiwemo miti ya minazi pamoja na korosho kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda pamoja na ujenzi wa bomba la Gas lakini hawana umeme wala maji safi ya kutumia

Ziara ya sambaChawene ililenga kutazama muendelezo kudhibiti  maji ya bahari ambayo yalitokana na mvua kali na hivyo kutoa maamuzi ya kuongeza nguvu kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali  ilikuweza kuyasogeza maji mbele na kiwanda kubaki salama.

Kutokana na Kazi iliyofanywa na jeshi la wananchii JWTZ ya kuweka vifusi na mawe limeweza kuzuia maji kufika eneo la kiwanda ambapo ilibaki mita 28 pekee kutoka mita 110 kwa bahari kufika eneo hilo la Kiwanda cha Mnazibay.

Kuhusu admin

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *