Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

- in Kitaifa, Mara

 

Na, Ahmed Makongo, Bunda;

WANANCHI wa kitongoji cha Mashine ya Maji katika kata ya Bunda stoo, mjini Bunda mkoani Mara, jana wamepiga yowe na kuanadamana kwa kukusanyika pamoja katika kituo cha Mashine ya kusukuma maji, iliyoko katika eneo la Migungani, mjini humo, kutokana na kituo hicho kufungwa na kusababisha kukosa huduma ya maji, kwa siku nzima ya jana.

Wananchi hao walifikia hatua hiyo baada ya kufika asubuhi katika eneo hilo, kwaajili ya kupata huduma hiyo ya maji na ndipo, wakakuta kituo hicho kimefungwa kwa kile kinachodaiwa kuwa mhudumu wa kituo hicho, ambaye ni mtumishi wa Idara ya maji, amekamatwa na polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili.

Ni kufuatia wananchi hao kufurika katika eneo hilo na kupaza sauti zao wakilalamikia kitendo hicho cha kukosa huduma hiyo ya maji mwenyekiti wa kitongoji cha Mashine ya Maji, Bw. Daud Kusekwa, amefika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwatuliza wananchi hao, ambao walikuwa na jazba, wakidai kuwa mhudumu wa kituo hicho amekamatwa bila kuwa na kosa lolote hivyo ni vyema akaachiwa uru.

Hali hiyo ya malalamiko ya wananchi hao ndiyo inayomfanya mwenyekiti huyo wa kitongoji kuamua kumuita afisa mtendaji wa kata ya Bunda Stoo, Bw. Raymond Bukombe na meneja wa mamlaka ya maji katika halmashauri ya mji wa Bunda, Injinia Mandemla Mansour, ambao wamefika katika eneo la tukio na kushuhudia umati mkubwa wa wananchi wengi wao wakiwa ni wanawake, waliokuwa tayari na vifaa vya kuchotea maji, lakini wakakosa huduma hiyo kutokana na kituo hicho kufungwa.

Hata hivyo, wananchi wa eneo hilo wakiongozwa na mwenyekiti wa kitongoji hicho, Bw. Daud Kusekwa, wamemuomba mkuu wa wilaya ya Bunda, Lydia Bupilipili, kuruhusu polisi wamuachie huru mtumishi wa idara ya maji.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Bodaboda watakiwa kuwafichua wahalifu.

JESHI la polisi mkoa wa kipolisi wa Tarime