Watu wanne washikiliwa Morogoro kwa jaribio la kuvamia kituo cha polisi

Watu wanne washikiliwa Morogoro kwa jaribio la kuvamia kituo cha polisi

- in Habari

picrobber-copy

Polisi mkoani Morogoro inawashikiria watu wanne wakazi wa Mzumbe wilayani Mvomero, kwa tuhuma za kujaribu kuvamia kituo cha polisi Mzumbe, baada ya kuwepo kwa taarifa za kufariki kwa mtuhumiwa mmoja aliyejulikana kwa majina ya Mustapha Aloyce, aliyekuwa akishikiriwa na Polisi kwa tuhuma za wizi.

Tukio hilo limetokea mara baada ya mtu huyo kuachiwa kwa dhamana, na baada ya kukaa siku tatu alifariki, kitendo kilichosababisha ndugu wa marehemu huyo, kubeba maiti yake na kuipeleka kituoni hapo, na Polisi kuipeleka Hospital ya Rufaa ya Morogoro tayari kwa uchunguzi, kitendo ambacho kimepingwa vikali na ndugu wa Marehemu.

Hata hivyo katika harakati za kuzuia vurugu hizo Polisi imelazimika kutumia mabomu ya machozi, na risasi za moto, hatua iliyopelekea watu wawili kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Hata hivyo jeshi la polisi mkoani limesema itaendelea kuwasaka wale wote waliohusika na tukio hilo, huku wakiwataka wananchi kuacha tabia ya kuvamia vituo vya Polisi, kwa lengo la kujichukulia sheria mkononi.

#StarTvTanzania

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

KESI YA SALUM NJWETE “SCORPION”: Shauri kusomwa Novemba 30 Ilala

Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion