Watuhumiwa TASAF wakamatwa.

Watuhumiwa TASAF wakamatwa.

- in Kitaifa, Rukwa

Takribani kaya 50 za wilayani Kalambo mkoani Rukwa zimeamriwa kukamatwa mara moja zikituhumiwa  kunufaika na fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kinyume na malengo ya mradi wa kusaidia kaya masikini.

Mradi wa kusaidia kaya masikini ukiwa na lengo la kuwapa fursa jamii iliyo katika lindi la umasikini umekuwa na changamoto nyingi lakini wilayani Kalambo Kaya hizo zaidi ya 50 zinadaiwa kujipatia fedha hizo pasipo sifa stahiki.

Kubainika kwa Kaya hizo kunatokana na uchunguzi wa kina uliofanywa Ofisi ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo na kubaini kuwa wapo watu ambao wameshindwa kubainisha maana ya neon umasikini bali walijipenyeza na kutoa taarifa zisizo sahihi ili waweze kujipatia fedha katika mradi huo wa TASAF, kama anavyoeleza Mratibu wa Mfuko huo Bw. Michael Mwasumbi.

Imeandikwa na,
Sammy Jumaa Kisika-Star Tv Rukwa.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

  Na, Ahmed Makongo, Bunda; WANANCHI wa kitongoji