Saturday , September 23 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Zanzibar / YURO MILIONI 3 zatengwa kwaajili ya mradi wa nishati mbadala Zanzibar

YURO MILIONI 3 zatengwa kwaajili ya mradi wa nishati mbadala Zanzibar

Kiasi cha yuro milioni tatu zinategemewa kutumika katika kufanikisha  upembuzi yakinifu wa mradi wa kutafuta umeme mbadala kwa zanzibar wa upepo na nishati ya jua ili kukabiliana na changamoto ya kutegemea umeme wa mfumo mmoja tu wa kutumia cable kutoka Tanzania Bara.

Fedha hizo kutoka Jumuiya ya Ulaya zinategemewa kuiwezesha Zanzibar kuwa na njia nyengine ya kupata nishati hiyo ambapo inakisiwa inaweza kupunguza gharama katika matumizi yake kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya warsha kwa wadau mbali mbali kuhusina na kujenga uwelewa namna ya uendeshaji na ufuatiliaji wa mradi huo visiwani zanzibar Naibu Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Maji, Nishati na Mazingira, Tahir Mohammed anasema kuwa hiyo ni fursa adhimu kwa zanzibar ambapo kwa kipindi kirefu Zanzibar haina uhakika wa upaikanaji wa nishati ya umeme kwa vile inatumia njia moja pekee  kutoka Tanzania Bara,

Meneja mradi huo kutoka shirika la umeme  Maulid Shirazi anasema kuwa watafanya utafuti wa kutosha na upembuzi yakinifu ili kuhakikisha kuwa inapatikana njia sahihi ya kupata umeme mbadala itakayoiwezesha Zanzibar kupata umeme wa uhakika sambamba na kutawanya elimu kwa jamii ili nao watambuwe mradi huo ambao tayari wameshaainisha maeneo ya kufunga minara.

Mada mbali mbali zimewasilishwa wakati wa warsha hiyo ambapo pia wadau walipata nafasi ya kuuliza na na kutoa michango ambayo kwa namna moja ama nyengine itafanikisha mradi hiyo.

Imeandikwa na Abdalla Pandu, Star TV – Zanzibar

Kuhusu Kisibi Isaya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *