Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Michezo na Burudani / Zidane atibuana na rais wa real Madrid Florentino Perez

Zidane atibuana na rais wa real Madrid Florentino Perez

zidane

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekwaruzana na rais wa klabu hiyo, Florentino Perez kabla ya kuanza kwa ziara ya maandalizi ya msimu ujao nchini Canada.

Ugomvi wao ulitokana na uamuzi wa Perez kulazimisha kinda wa miaka 17, Martin Odegaard aliyesajiliwa Januari ajumuishwe kwenye kikosi kilichosafiri na kufanya ziara Amerika Kaskazini.

Zidane anaiongoza Real Madrid kuzuru Canada kwa maandalizi ya msimu ujao akiwa amefuatana na wanae, Luca na Enzo.

Kocha huyo alidhamiria kumtoa kwa mkopo kinda huyo akiamini kuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Baada ya Zidane kueleza hakuna nafasi kwa kinda huyo, Perez aliibuka na kusisitiza lazima aende, hivyo kuzua msigano wa kwanza baina yao tangu kocha huyo aanze kazi Januari, mwaka huu.

Perez alimtaka Odegaard kwenye ziara hiyo ya Amerika Kaskazini kwa sababu ameandikiwa kwenye mkataba wake kuwa ni mchezaji wa kikosi cha kwanza akiamini angeweza kumpatia klabu.

Baada ya ugomvi huo, Odegaard alipanda ndege na wenzake na kutua salama Montreal ambako ikiwa Canada, itacheza dhidi ya klabu za huko, ingawa Zidane hakupendezwa na uamuzi huo.

Vyombo vya habari vya Ufaransa, ikiwamo Le10Sport vilieleza kuwa Perez alilazimisha Odegaard kuwamo kwenye kikosi cha Real Madrid kinachozuru Canada jambo ambalo halikumfurahisha Zidane.

Madrid inajiandaa kwa msimu mpya baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Arusha wasusia uchaguzi wa viongozi

Chama cha riadha mkoa wa Arusha kimepinga kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa shirikisho la …

Kuimarishwa uwanja wa Nyamagana

Mipango ya kuendeleza soka la vijana huenda ikawa na tija endapo tu serikali chini ya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *